Back to top

Watumishi 2 kuswekwa ndani kutokana na matumizi mabaya ya fedha.

16 March 2021
Share

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Tekinolosia Mhe.Omari Kipanga amemwagiza mkuu wa wilaya ya Nkasi Saidi Mtanda kuwaweka ndani watumishi wawili akiwemo mkuu wa chuo cha maendeleo ya jamii cha Chala pamoja na katibu wa kamati ya ujenzi wa chuo hicho kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za serikali.

Naibu huyo pia ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuzichunguza kamati 3 za ujenzi wa chuo hicho kutokanana matumizi mabaya ya fedha za serikali yaliyo sababisha chuo hicho kujengwa chini ya kiwango.

Akiongea wakati wa ziara yake ya kutembelea chuo hicho, amesema ujenzi wa chuo umejengwa chini ya kiwango na kusisiza kuundwa kwa tume ya kuchunguza ubadhifu wa fedha.

Mkuu wa wilaya hiyo Saidi Mtanda amesema ubadhirifu hupo umetokana na usimamizi mbovu wa miradi hiyo.