
Watumishi 28 wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, wamefunguliwa mashtaka na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), wakituhumiwa kughushi nyaraka kwa ajili ya wategemezi wao, na kupelekea hasara ya zaidi ya Tsh.Bil. 1 kwa mfuko huo, huku wengine wakiendelea kusakwa ili kufikishwa mahakamani.
.
Hata hivyo, Mfuko huo umebainisha kuwa Watumishi hao pia wameandikiwa barua kila mmoja wakitakiwa kurejesha fedha hizo, kwani wanufaika hao hawakustahili.
