Back to top

Watumishi 5 mbaroni kwa wizi wa vifaa vya ujenzi Mwanza.

24 July 2021
Share

Watumishi watano wa Halmashauri ya wilaya Buchosa mkoani Mwanza wanashikiliwa na jeshi la polisi wilayani humo kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa vifaa mbalimbali vya ujenzi wa nyumba za watumishi wa halmashauri hiyo akiwemo mtunza stoo, wahasibu wawili na mlinzi.

Watumishi hao watano wamekamatwa baada ya vifaa mbalimbali vya ujenzi vinavyodaiwa kuibwa kwenye stoo ya halmashauri ya Buchosa  kupatikana vikiwa vimehifadhiwa katika nyumba moja iliyoko kijiji cha kayenze kata ya nyehunge mali ya taifa pambano iliyoko mita chache kutoka jengo la halmashauri vinavyodaiwa kuibwa kwenye stoo ya halmashauri hiyo.

Jitihada za kubaini vifaa hivyo vilipohifadhiwa zilifanywa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na Mbunge wa Buchosa Erick Shigongo.

Mkuu wa wilaya Sengerema Senyi Ngaga amethhibitishwa kukamatwa kwa watumishi wanaotuhumiwa kujihusisha na wizi wa vifaa hivyo.