Back to top

Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wakumbushwa wajibu na majukumu yao.

25 June 2020
Share

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi.Doroth Mwaruko amewakumbusha watumishi wa Ofisi yake wajibu wa majukumu yao wawapo kazini na kuwataka kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa kila moja kwenye eneo lake.

Katibu Mkuu amesema hayo kwenye mkutano na watumishi wa Ofisi yake katika kukamilisha wiki ya uttumishi wa umma kwa mwaka 2020 iliyo beba kauli mbii isemayo “Jukumu la mtumishi wa umma katika kujenga na kudumisha amani iliyopo miongoni mwa jamii”

Katika kikao hicho aliwakumbusha kuwa na nidhamu ya kutosha katika uwajibikaji wa kazi na kila mtumishi kuzingatia sheria na taratibu za kazi awapo kazini.

Aidha aliwakumbusha pia watumishi kukamilisha ujazaji fomu za upimaji utendaji kazi yani (OPRAS) ambacho ndicho kipimo sahihi cha uwajibikaji wa mtumishi wa umma.

Naye mkurugenzi wa utawala na Rasilimali watu Bw:Greyson Mwaigombe alimshukuru Katibu Mkuu kwa niaba ya watumishi wote na kuhaidi kutekeleza yale yote aliyoelekeza.

Mkutano huo ilifanyika katika ukumbi wa hazina jijini Dodoma huku ukihudhuriwa na watumishi wote wa Ofisi ya waziri Mkuu na Mada mbalimbali zilitolewa kuwakumbusha watumishi namna ya uwajibukaji na kuzingatia maadili ya kazi na usalama mahala pakazi.