
Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu, amewataka watumishi wa Afya kufanya kazi kwa kuzingatia taaluma, Maadili na weledi katika kazi zao.
Waziri Ummy ametoa kauli hiyo alipotembelea Hospitali ya Wilaya ya Mbozi iliyopo Mkoa wa Songwe na kujionea hali ya utolewaji wa huduma za Afya, upatikanaji wa dawa pamoja na maendeleo ya miradi ya ujenzi katika Hospitali hiyo.
Waziri Ummy yuko Wilaya ya Mbozi katika ziara ya siku Tatu, ambapo ataendelea kukagua huduma zinazotolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe pamoja na upatikanaji wa dawa katika Hospitali hiyo.
