
Serikali imewapiga marufuku watumishi wa afya nchini, kutumia simu na kufanya mazungumzo binafsi wakati wa kazi katika vituo vya kutolea huduma za afya.
.
Marufuku hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu, baada ya kuongezeka kwa malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu udumavu wa huduma katika vituo vya afya, huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni watumishi wa afya kutumia muda mwingi kuchati na kufanya mawasiliano ya kibinafsi kupitia simu zao za mkononi badala ya kuzingatia majukumu yao ya kitaalamu.
.
Aidha, Prof. Nagu, amewasisitiza watumishi wa afya kuzingatia majukumu yao ya kitaalamu wakati wote wa kazi ili kuhakikisha wanatoa huduma bora na zenye ufanisi kwa wananchi.
