Back to top

WATUMISHI WA ARDHI MSIUZE UTU KWA VITU VIDOGO

09 April 2024
Share

Naibu Waiziri Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda, amewataka watumishi wa Wizara ya Ardhi kutembea kifua mbele na kuacha kuuza utu wao kwa vitu vidogo vidogo.

Naibu Waziri Pinda amesema hayo Jijini Dodoma, na kuwahimiza watumishi wa sekta ya ardhi kutotoa huduma kwa kuangalia hali za watu na badala yake wafanye kazi kwa kuzingatia haki.

Mhe.Pinda amewakumbusha watumishi hao kufanya kazi kwa utiifu na kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu kutoka kwenye vitakatifu na kwa hakika watabarikiwa.

Aidha amewafikishia salamu za pongezi kutoka kwa Rais Samia kwa kupongeza mabadiliko makubwa ya kiutendaji ya Wizara ambapo amewataka watumishi hao kutobweteka ili kuyaishi maono ya Rais Samia Suluhu Hassan.  

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Bi.Lucy Kabyemera, amesema watumishi wanafarijika sana wanapoona viongozi wakuu wa Wizara wanafika kwenye matukio muhimu na kuwakumbusha juu ya utendaji