Back to top

Watumishi wa sekta ya Madini watakiwa kufanaya kazi kwa weledi.

08 May 2018
Share

Waziri wa Madini Mh.Angellah Kairuki amewataka watumishi wa sekta hiyo kuhakikisha wanafanya kazi kwa uadilifu na weledi mkubwa na kutoa elimu kwa umma na wadau mbalimbali ambao wanania ya kuwekeza katika sekta hiyo ili kuhakikisha wanatoka katika asilimia 4.8 ya mchango wa taifa badala yake wafike asilimia 10 katika kuchangia pato lataifa.

Waziri Kairuki ameeleza hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa baraza la wafanya kazi uliofanyika mkoani Morogoro lengo likiwa ni kujadili mada mbalimbali kuhusu umuhimu wa baraza la wafanyakazi muundo wa wizara ya madini na maadili katika utumishi wa umma, mapitio ya tekelezaji wa bajeti ya mwaka 2017-2018, mpango wa bajeti wa mwaka 2018-2019 pamoja na marekebisho ya sheria ya madini ya mwaka 2017.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati Madini Profesa Idris Kikula ameeleza kuwa leseni za wachimba madini zaidi ya 8000 zipo tayari hivyo waliokidhi vigezo wanatakiwa walipie ili waweze kupewa leseni hizo huku katibu mkuu Wizara ya Madini akieleza kuwa watatoa elimu kwa wafanyakazi wanaotarajia kustaafu ili waweze kujikimu kimaisha bada ya kustaafu.