Back to top

Watumishi wa serikali watakiwa kuwa waaminifu.

19 September 2018
Share

Watumishi wa serikali wametakiwa kuwa waaminifu kwa kufanya kazi kwa bidii, ili waweze kufikia malengo yaliyo wekwa na serikali kwa wakati.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dakta Rehema Nchimbi ametoa agizo hilo wakati akikabidhi pikipiki kwa waratibu elimu kata wa halmashauri ya wilaya ya Singida na kuwataka kutumia pikipiki hizo kuwakagua walimu na kuongeza ufaulu.

Awal, Ofisa Elimu Shule za Msingi halmashauri ya wilaya ya Singida Bwana Sepeku Kinyemi amesema maofisa elimu kata ishirini na mmoja wanapatiwa pikipiki ili kuboresha elimu kwenye kata zao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Singida Mheshimiwa Elia Digha amewakumbusha waratibu kata elimu, kuwa pikipiki walizopewa zisiwafanye wawe vilema kwa kuendesha bila kuzingatia sheria.

Mwenyekiti wa waratibu elimu kata Bwana Christopher Philipo amehadi kwa niaba ya wenzake kuwa watatumia pikipiki kwa malengo yaliyo kusudiwa.