Back to top

WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUENDANDA NA MAHITAJI YA SASA

25 November 2022
Share


Vyuo vya utumishi wa umma nchini vimeagizwa kufanya tafiti, na kuboresha mafunzo kwa kuzingatia mahitaji yaliyopo lengo likiwa watumishi wa umma, waendane na maitaji ya uchumi yalipo kwa sasa.

Akizungumza katika mahafali hayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma, Mhe.Jenista Mhagama amesema kuna kila sababu kwa vyuo vya utumishi wa umma kufanya utafiti mbalimbali ili kuboresha mafunzo kwa kuzingatia mahitaji yaliypo.

Amesema mambo ambayo ni kipaumbele hayana budi kufanyiwa utafiti wa kina, ili watumishi wa Umma, waweze kubadilika na walingane na mahitaji ya aina ya utumishi wa umma katika uchumi uliyopo sasa.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha Utumishi wa Umma mkoani Mtwara, Emmanuel Shindika amesema mahafali hayo ya thelathini na sita yamekuwa na wahitimu miasita na kumi na tano wanawake wakiwa elfu tatu na miasaba na 37, huku wanaume wakiwa elfu mbili miatano na sabini.