Back to top

WATUMISHI WANAOTOA LUGHA CHAFU WAONYWA

22 March 2024
Share

Naibu Katibu Mkuu, OR-TAMISEMI, Dkt. Charles Mahera, amesema kumekuwepo na taarifa za baadhi ya watoa huduma za Afya katika Hospitali ya Mji wa Tarime kutumia lugha chafu kwa wagonjwa na kutotoa huduma bora kwa wananchi, jambo ambalo amesema halikubaliki na ni kinyume na utaratibu wa sheria za kitabibu.
.
Dkt. Mahera ameyasema hayo wakati akizungumza na Timu za Usimamizi wa Huduma za afya za Mkoa na Halmashauri kwa lengo la kujadili hali ya utoaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime.
.
Amesema, Timu za usimamizi huduma za afya zinatakiwa kusimamia na kuhakikisha kuwa zinabadilisha tabia za watumishi wa aina hiyo kwani hawapo juu ya sheria bali wameajiriwa na Serikali kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wananchi. 
.
Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan amewekeza fedha nyingi kwenye miundombinu, vifaa na vifaa tiba ni wajibu wa kila mtumishi wa afya kutoa huduma bora kwa wananchi ili kuwaokoa maisha ya watu.
.
Pia amewataka kuboresha hali ya utoaji wa huduma na kuacha tabia kuleana na kutaka kuwafichua wasiotekeleza wajibu wao ipasavyo ili sheria ichukue mkondo wake na watu kama hao hawahitajiki.