Back to top

Watumishi wanne wasimamishwa kazi, watendaji 30 wakamatwa.

23 June 2020
Share

Mkuu wa Mkoa Kagera Brig.Jen. Marco Gaguti amemwagiza kamanda wa polisi mkoani humo  na Kamanda wa TAKUKURU kuwakamata watumishi 34 katika Halmashauri ya wilaya Biharamulo wakiwemo watendaji wa Vijiji na Kata kwa kushindwa kurejesha fedha shiligi milioni 307 zilizokusanywa kutoka vyanzo vya mapato ya ndani bila kupelekwa Benki.

Agizo hilo amelitoa  alipofanya ziara ya kikazi wilayani humo iliyolenga kutoa maelekezo ya kiutendeji kutokana na halmashauri hiyo kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato na kuoneka kunaubadhilifu wa fedha za serikali.

Mkuu huyo pia licha ya kuagiza kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi watumishi hao, ameziagiza mamlaka kuwasimamisha kazi Kaimu Mwekahazina Sospeter Makene, Justine Banula Afisa Tehama, Rogers Semukoko Afisa Tehama na Beatrice Gurusya Afisa Biashara wote wakiwa ni watumishi wa halmashauri hiyo.

Gaguti amechukua uamuzi huo baada ya kutoa siku saba kwa watumishi hao kurejesha fedha hizo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika juni 05 mwaka huu kilichokuwa kina lengo la kujibu hoja za mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali.