Back to top

Watumishi watatu Itigi wafukuzwa kazi kwa kugushi vyeti. 

22 May 2020
Share

Baraza la madiwani la halmashauri ya Itigi wilayani Manyoni limewafukuza kazi watumishi watatu  mhandisi , daktari  na muuguzi wa halmashauri hiyo baada ya  kubainika kugushi vyeti vya uhandisi na kidato cha nne.
 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi Bw. Ally Minja amesema hayo kwenye baraza la madiwani la halmashauri kuwa watumishi hao  walifukuzwa kazi baada ya kusimamishwa  kwa muda mrefu  na baada  ya baraza kuridhika limepitisha uamuzi huo.