
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa ameelekeza kusimamishwa kazi kwa watumishi wawili wa Wizara yake ili kupisha tuhuma zinazo wakabili.
Watumishi waliosimamishwa kazi ni Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Simiyu Salvatory Lutaba na Mke wake ambaye ni Msajili wa Hati mkoa wa Mwanza Levina Kayandaga.
Waziri Silaa amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara yake kuwasimamisha kazi watumishi hao leo jijini Mwanza wakati alipofanya ziara katika eneo lenye mgogoro wa umiliki wa ardhi mtaa wa Nyamhongolo wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.
Maelekezo hayo ameyatoa Waziri Silaa baada ya kusikiliza pande mbili za walalamikaji kwa takriban siku tatu mfululizo kuhusu mgogoro wa viwanja viwili namba 863 na 864 vyote vipo mtaa wa Nyamhongolo wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.
