Back to top

Watumishi wawili wa TANROADS mzani Muleba matatani kwa rushwa.

17 January 2020
Share

Taasisi ya Kuzuia na rushwa nchini (TAKUKURU) imewakamata watumishi wawili wa Wakala wa barabara (TANROADS) wanaofanya kazi katika mzani wa kupima uzito wa magari ulioko eneo la Kyamyolwa lililoko wilayani Muleba kwa tuhuma ya kupokea rushwa kutoka kwa wamiliki na madereva wa magari yanayozidisha uzito. 
 
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa ofisini kwake Mkuu wa TAKUKURU katika mkoani Kagera, John Joseph amewataja watumishi waliokamatwa na taasisi hiyo kuwa ni pamoja na Damas Simemba na Reuben Mgoya.