
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki ameagiza Wananchi wote wanaofanya shughuli mbalimbali za kibinadamu kwenye eneo lenye zaidi ya ekari 5000 lililokuwa likitumika kupumzishia mifugo “Chibe holding ground” lililopo Wilayani Shinyanga mkoani Shinyanga kuondoka ifikapo Agosti 30 mwaka huu.
.
Mhe. Ndaki ameyasema hayo baada ya kufika na kukagua eneo hilo ambapo amewataka wananchi wanaolitumia eneo hilo kwa shughuli za kilimo kuhakikisha wameondoka baada ya mavuno ya mazao yao ambayo kwa wakazi wa mkoa huo huwa ni kati ya mwezi Aprili hadi Agosti.
