Back to top

Wavusha mazao kwa kubeba kichwani Momba.

19 May 2020
Share

Wananchi katika kijiji cha Ntinga Kata ya Msangano wilaya Momba mkoani Songwe  wanalazimika kujitwisha mazao kichwani ili kuyavusha kwenye mto  Nkana kwa kile kinachoelezwa  ukosefu wa daraja la kiteputepu .

Wamedai kuwa mazai yanahofiwa kuharibika kutokana na hali hiyo.


Aidha sehemu zote za kuvuka kwa kutumia Ngalawa hazijawa msaada kwa wakulima kutokana na wapiga Makasia kutoza bei kubwa za nauli.


Ukanda huo unaoanzia milima ya Mbozi umekatika madaraja 7 ya viteputepu kwenye mto Nkana na mto Momba miezi 4 iliyopita kutokana na Mvua kubwa zilizonyesha kwa takribani siku 6 mfululizo. 


Mkuu wa wilaya Momba Juma Said Irando amesema ujenzi ni wa madaraja hayo ulikwama kutokana na mvua  endelevu.