Back to top

WAVUVI WADOGO WAMPA MAUA YAKE RAIS SAMIA

07 June 2024
Share

Wavuvi wadogo hapa nchini wamesema wanaona fahari kutembea kifua mbele kwa sababu ya mipango mizuri ya Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan aliyoiweka juu ya kuwasaidia kuinuka na kuboresha shughuli zao.

Hayo yamebainishwa na mwakilishi wa wavuvi wadogo hapa nchini, Feisal Mohamed Ali, wakati akitoa salamu kwenye Mkutano wa Wavuvi Wadogo Afrika uliofanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 5-7,2024.

Amesema jitihada zote hizo zinazofanywa na Rais Samia ni ishara ya nia yake thabiti ya kutaka kumuinua mvuvi hapa nchini.

Amefafanua kwa kusema kuwa nia njema ya rais Samia ya kutaka kumuinua mvuvi inajidhirisha pia katika kiasi cha bajeti anachokitenga kwa ajili ya wizara ya mifugo na uvuvi ambayo imekuwa ikipanda kuanzia mwaka 2021 kutoka bilioni 73 mpaka kufikia bilioni 330 mwaka wa fedha 2024/2025 ikiwa ni ongezeko la asilimia 600 kwa muda wa miaka 3.

Amebainisha kuwa kufuatia dhamira njema hiyo aliyonayo rais samia kwa wavuvi, ahadi yao kwake ni kuendelea kumuunga mkono yeye pamoja na hawata muangusha.