Back to top

WAWEKEZAJI WA NDANI WACHANGAMKIE FURSA.

17 October 2022
Share

Serikali imewataka wawekezaji wa ndani na nje wachangamkie fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania katika sekta mbalimbali.

Taarifa ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa vyombo vya habari imesema Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Mwigulu Nchemba, ametoa wito huo mjini Washington, Marekani, alipozungumza na Mkurugenzi anayesimamia masuala ya masoko ya mitaji, maendeleo ya Nishati na Mabadiliko ya Tabia Nchi wa Benki ya Dunia Bw.Sarvesh Suri.

Amesema serikali inaendelea kuboresha mazingira rafiki ya uwekezaji na biashara ili kuchochea uwekezaji na kuvutia mitaji na Teknolojia kutoka nje ya nchi, na kuiomba taasisi hiyo itoe dhamana kwa kampuni, taasisi au mashirika yanayotaka kuwekeza nchini Tanzania.

Kwa upande wake, Bw.Suri ameipongeza Tanzania kwa hatua zake za kuboresha mazingira ya uwekezaji ambayo yameanza kuwavutia wawekezaji wengi wanaotaka kuwekeza nchini kupitia taasisi yake.