Back to top

Wawekezaji waiomba serikali kudhibiti uvamizi wa Tembo.

07 June 2021
Share

Wawekezaji waliowekeza kwa zaidi ya miaka kumi na tatu katika vitalu vya ranchi za taifa wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kudhibiti uvamizi wa Tembo katika vitalu vyao pamoja na kudhibiti baadhi ya wananchi wanaovamia ranchi za taifa na kufanya shughuli za kibinaadamu hali ambayo imekuwa kikwazo katika kuendeleza sekta ya mifugo.

Wawekezaji hao wametoa kilio hicho mbele ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki ambapo wameiomba serikali kuingilia kati suala la wananchi kuvamia maeneo yao waliyowekeza.

Kwa upande wake katibu wa umoja wa wawekezaji hao Dr.Emmanuel swai ameiomba serikali kuingilia kati suala la mikataba yao ambayo imekuwa si rafiki kwa wawekezaji.
 
Akitoa ufafanuzi wa hoja za wawekezaji hao, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki amesema kuwa serikali ipo pamoja na wawekezaji hao na itachukua hatua kali kwa wale wote wanaovamia maeneo ya ranchi kinyume na sheria.