Back to top

Wawekezaji waliochukua mikopo ya magumashi Arumeru kukiona.

13 June 2021
Share

Waziri wa Kilimo Prof.Adolf Mkenda amesema Serikali haitawavumilia wawekezaji waliochukua mikopo ya magumashi na kutelekeza mashamba 16 ya maua na mboga Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.

Waziri Mkenda ameyasema hayo alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo alipotembelea na kukagua mashamba yenye ukubwa wa Hekari 1, 950 Wilayani Arumeru.

Amesema wawekezaji hao walichukua mikopo lakini wameshindwa kurejesha mikopo hiyo na kuisababishia serikali hasara tangu mwaka 2018.

Waziri Mkenda amesema kuwa Mashamba hayo kwa mwaka mmoja yanapoteza dola za Kimarekani zaidi ya milioni 24 na ajira 6, 700 kwa mwaka.

Akizungumzia mashamba hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi Kilele ya mazao ya maua na mboga Dkt.Jacqueline Mkindi amesema kutelekezwa kwa mashamba hayo kumepoteza ajira 6, 700 za Watanzania na kuisababishia Serikali hasara kubwa ya mapato.