Back to top

WAWILI MBARONI WAKITOROSHA MIFUGO, ARUSHA

07 April 2024
Share

Jeshi la Polisi, Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo kwa kushirikiana na wananchi limewakamata watuhumiwa wawili wakitorosha mifugo 514, kwenda Nchi jirani huku wakitumia vibali vya kampuni isiyohusika na mifugo hiyo.
.
Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo nchini, SACP Simon Pasua, amesema Aprili 06, 2024 waliwakamata watuhumiwa hao, ambao majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi, wilayani Longido, mkoani Arusha, wakiwa na mifugo hiyo, ambayo walikuwa wakiitorosha kwenda nchi Jirani.
.
Aidha, Kamanda Pasua amewaomba wananchi kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na utoroshaji pamoja na kukiuka taratibu za uuzaji wa mifugo hapa nchini.