Back to top

Wawili wakamatwa wakiwa na nyama ya pofu.

03 March 2022
Share

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishina Msadizi wa Polisi ACP Justine Masejo amesema jeshi hilo limewakamata watu wawili ambao ni Amanda Thomas (22) mkazi wa Morombo na Kelvin Thomas (27) mkazi wa Ngarenaro wakiwa na nyama Pori ya mnyama Pofu Kilo 150 katika eneo la Ngarenaro katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Kamanda Masejo amesema kuwa uchunguzi wa awali wa tukio hili umebaini kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakijihusisha na biashara hiyo ya nyara za serikali ambapo uchunguzi unaendelea kwa kushirikiana na askari wanyama Pori ili kubaini mtandao wao.

Kamanda Masejo katika tukio jingine katika kata ya Rhotia tarafa ya Mbulumbulu wilaya ya Karatu na Mkoa wa Arusha askari Polisi walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili ambao ni Petro Gaudence (57) na Revocatus Protus (28) wakazi wa Mbulumbulu wakiwa na lita 570 za gongo.