Back to top

Wawili washikiliwa na Polisi Morogoro kwa kukutwa na Pembe za Ndovu.

16 May 2018
Share

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu wawili kwa makosa mawili tofauti akiwemo mmoja kwa kukamatwa na Pembe za Ndovu mbili za thamani ya shilingi milioni 34 na mwingine kwa kukutwa na Katoni 56 za Vipodozi vilivyopigwa marufuku.

Watuhumiwa waliokamatwa ni Joel Amos mkazi wa Mikumi aliyekutwa na Pembe mbili za Ndovu zenye uzito wa gramu kumi, za thamani ya shilingi milioni 34 na Bibiana Mwita mkazi wa Kitunda Dar es Salaam  aliyekutwa na Katoni 56 za vipodozi vilivyopigwa marufuku nchini ambapo kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Urlich Matei amesema kukamatwa kwa Joel kumefanywa na polisi kwa kushirikiana na maafisa Wanyama Pori.
 
Kamanda Matei amesema Katoni za Vipodozi zimekamatwa eneo la Melela majira ya usiku ambapo vilikuwa vimefichwa katika mifuko ya Plastiki kwenye gari na watuhumiwa wote wanahojiwa na polisi wakitarajiwa  kufikishwa mahakamani mara upelelezi ukikamilika.