Back to top

Wazalishaji wa nguzo watakiwa kuongeza uzalishaji.

24 June 2020
Share

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu uwekezaji Mhe.Angela Kairuki ameyataka makampuni yanayozalisha nguzo za umeme kuongeza uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya bidhaa hiyo ambayo imekuwa na umuhimu mkubwa kutokana na ujenzi wa miradi ya umeme vijijini unafanywa na (REA)

Waziri Kairuki ametoa rai hiyo alipotembelea kiwanda cha uzalishaji nguzo za umeme Qwihaya General Enterprises kilichopo wilayani Mufindi.

Benedict Mahenda ni kaimu mkurugenzi wa kampuni anasema moja ya changamoto katika biashara hiyo ni ubovu wa barabara.