Back to top

WAZAZI WATAKIWA KUWALINDA WATOTO.

03 June 2023
Share

Wazazi na walezi, wametakiwa kuwalinda watoto wao kama wanavyolinda mali nyingine, ili kuwaepusha dhidi ya kufanyiwa vitendo vya kikatili ikiwemo ubakaji na ulawiti.

Hayo yamesemwa na Waziri  wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalum, Mhe.Dk. Dorothy Gwajima  wakati akizindua Kampeni  ijulikanayo kwa jina la ‘‘Sema Nao’’ iliyoandaliwa na Jeshi la Polisi kwa lengo la kuelimisha Jamii katika masuala ya kiuhalifu hususani ya ukatili wa Kijinsi.

Waziri Gwajima pia amewataka watoto kukataa zawadi wanazopewa na watu wasiowafahamu ama wanapoitwa na watu wasiowafahamu kutokana na mbinu hizo hutumiwa na watu wabaya na kuwarubuni.

Kampeni hiyo imezinduliwa katika viwanja vya Shule ya Msingi Ihumwa Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na wanafunzi,  viongozi wa Serikali, wananchi pamoja na Maafisa toka Jeshi la Polisi.