Back to top

Wazazi,walezi wahimizwa kuvaa barakoa wanapopeleka watoto kliniki.

20 May 2020
Share

Wazazi na walezi wamehimizwa kuzingatia kuvaa barakoa kila wanapowapeleka watoto wao hospitalini, vituo vya afya na zahanati kupatiwa huduma mbalimbali za kiafya ikiwamo zile za chanjo.

Rai hiyo imetolewa na Ofisa Miradi kutoka Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Chanjo (IVD), Dk. Furaha Kyesi alipozungumza na wazazi na walezi waliofika katika Zahanati ya Madizini iliyopo Kata ya Mtibwa Wilayani Mvomero mkoani Morogoro kupata chanjo na kupima uzito wa watoto wao.