
Wazee wa klabu ya Simba wamemuomba Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ampeleke CAG kupitia na kuikagua Klabu ya Simba ikiwemo kupitia sheria kandamizi na za kibaguzi katika michezo.
Wazee hao wameonesha kutokubaliana na Mkutano mkuu wa Klabu hiyo Jumapili unaotarajiwa kufanya mabadiliko ya katiba wakidai mkutano huo ni batili kwani viongozi wa klabu hiyo wamekwisha ibadili katiba wao peke yao na wanachotaka ni wanachama kuipitisha tu kinyume na sheria inavyowataka kuunda rasimu kwanza na wanachama waisome watoe mawazo yao ili ipitishwe na kuwa Katiba.
Wazee hao Wamepinga rasimu ya Katiba ya klabu hiyo toleo la mwaka 2016 wakidai imepitishwa kinyume na sheria za nchi wanataka itambulike Katiba ya mwaka 2014.