Back to top

Wazee wa Mbesa Tunduru walalamika kunyimwa mikopo na taasisi za fedha.

15 October 2018
Share

Baadhi ya wazee wa kijiji cha Mbesa katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, wamezilalamikia taasisi mbalimbali za kifedha kwa kushindwa kuwapa mikopo kwa madai wazee hawakopesheki na kwamba kitendo hicho kinawanyima fursa ya kujiendeleza kiuchumi kwenye vikundi vyao ikiwa ni pamoja na kumudu gharama mbalimbali za kimaisha.


Baadhi ya wazee hao waliopo kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF), wamedai licha ya kujiunga na kujisajiri na vikundi vya uzalishaji mali lakini kasumba kubwa wanayoipata ni kukosa fursa za mikopo kutoka kwenye taasisi za kifedha.