
Wazee wanaotunzwa katika Kituo cha Kulea Wazee Silabu Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma wameiomba serikali na wadau wa maendeleo kuona uwezekano wa kuezeka upya nyumba zao ambazo zinavuja kipindi cha mvua na maji kuingia ndani na hivyo kuwasababishia adha ya kuishi katika mazingira magumu.