Back to top

WAZIRI AWESO ANADI MIRADI YA MAJI KOREA

07 December 2024
Share

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso amefanya mazungumzo na Benki ya EXIM ya Korea ambayo ilitoa fedha za utekelezaji wa miradi ya majitaka nchini Tanzania, yenye jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 248.3.

Utelezaji wa miradi hiyo utaimarisha huduma za usafi wa mazingira, kuondoa na kutibu majitaka, ambapo pia Tanzania imepata msaada wa Dola za Kimarekani milioni 8 ambazo zitajenga mfumo wa kusimamia huduma za maji (Smart Water Management System) katika Mamlaka ya Maji Iringa kutoka Korea Environmental Industry and Technology Institute (KEITI). 

Pia, Kupitia mfumo huo, IRUWASA itakuwa Mamlaka ya Maji ya kwanza nchini kutumia mfumo huo ambao utaongeza ufanisi katika kudhibiti upotevu wa maji, kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kuimarisha huduma ya maji.

Aidha, Makamu wa Rais wa Benki hiyo amesema kupitia EDCF na Mifuko mingine Serikali ya Korea itaendelea kuisapoti Serikali ya Tanzania kupitia Sekta ya Maji katika uwekezaji zaidi wa utejelezaji wa Miradi ya Maji.