Back to top

Waziri Bashungwa ataka vituo vya huduma kwa wateja kila mkoa.

18 January 2022
Share

Waziri wa TAMISEMI Mh. Innocent Bashungwa amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Riziki Shemdoe kuweka mikakati ya uanzishwaji wa vituo vya kutolea huduma kwa wateja kwa kila Mkoa ili kurahisisha utoaji wa Huduma bora kwa wananchi.
.
Waziri Bashungwa ametoa maagizo hayo alipotembelea Kituo cha Huduma kwa wateja cha Ofisi ya Rais –TAMISEMI kwa lengo la kuangalia maelekezo aliyoyatoa kuhusu maboresho ya kuhakikisha huduma bora inatolewa kwa wananchi.