
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabuka amewataka wananchi wote wanaonunua ardhi kufanya uhakiki kabla ya kununua kupitia ofisi za Halmashauri sambamba na kufanya Search kwa maeneo yaliyo na hati.
Dkt Mabula amesema hayo wilayani Kibaha wakati alipokwenda na Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mashimba Ndaki kupokea na kukabidhi taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa ardhi katika eneo la kiwanja namba 34 Pangani Kibaha chenye ukubwa wa hekta 1037 ambapo wananchi 1002 wamebainika kuvamia kiwanja cha eneo hilo linalomilikiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi chini ya taasisi yake TVLA.
"Ntoe rai kwa wananchi wote wanaonunua ardhi kufanya uhakiki kabla ya kununua kupitia ofisi za Halmashauri na kufanya Search kwa maeneo yaliyo na hati’’ alisema Dkt Mabula.

