Back to top

WAZIRI MABULA AKABIDHI SCANNER 50 KURAHISISHA KUMBUKUMBU ZA ARDHI.

23 June 2022
Share

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula amekabidhi Scanner 50 zenye thamani ya shilingi milioni 880 kwa kwa ajili ya kurahisisha zoezi la kubadilisha kumbukumbu za ardhi kutoka analogia kwenda digitali.

Dkt.Mabula amekabidhi sehemu ya Scanner hizo kwa Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Tabora Jabir Singano kwa niaba ya mikoa mingine wakati akiwa katika ziara yake ya siku moja katika mkoa wa Tabora.

Scanner zilizokabidhiwa zitasambazwa kwenye mikoa ya Mwanza scanner 9, Kagera 5, Tabora 6, Songwe 7, Dodoma 9, Shinyanga 7 na Mbeya 7 ambazo zote zinapelekwa kusaidia zoezi zima  linaloendelea kwenye mikoa hiyo.

Akizungumza wakati wa kukabdhi vifaa hivyo, Dkt.Mabula alisema kuwa, uamuzi wa wizara yake kutoa vifaa hivyo ni kutaka kuharakisha zoezi zima la kubadilisha kumbukumbu za ardhi kutoka analogia kwenda digitali.

"Tunatarajia sasa ninyi mliokabidhiwa jukumu hili la kubadilisha kumbukumbu kwa niaba ya wengine wote nchi nzima mtaendelea kuifanya kazi hii kwa weledi na kuongeza kasi ili tumalize na kuondokana na masuala ya mavumbi ya kwenye ‘mafile’ na tucheze na mfumo"Amesema Dkt.Mabula