Back to top

WAZIRI MAJALIWA AKAGUA UWEKAJI ALAMA LOLIONDO.

23 June 2022
Share

Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa amekagua kazi ya uwekaji alama za kubainisha eneo la hifadhi lenye ukubwa wa Kilomita za mraba 1500 katika eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro, Mkoa wa Arusha. 

Mhe.Majaliwa amezipongeza Taasisi zote zilizokuwa zinaratibu zoezi la uwekaji wa alama katika eneo la pori tengefu la Loliondo kwa kukamilisha uwekaji wa vigingi 424 vilivyokusudiwa kuwekwa.

"Ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini unatokana na kodi ambazo Serikali inakusanya kutoka maeneo tofauti ikiwemo sekta hii ya utalii"Amesema Waziri Mkuu.

Amesema kuwa Watanzania hawana budi kuzingatia na kuzifuata sheria zilizowekwa. “Kila nchi ina utamaduni wake, hata wewe Mtanzania unapotoka kwenda nchi yoyote, fuata sheria za nchi hiyo".

Amesema kuwa zoezi lililofanyika ni uwekaji wa alama tu, na hakuna mtu yeyote atakayeondolewa katika vijiji vinavyozunguka eneo hilo. “Hili eneo liko umbali wa karibu kilomita 12 hadi 15 kutoka kwenye makazi ya watu".

Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa zoezi la ulinzi katika eneo hilo ni endelevu katika kipindi chote na si wakati huu wa uwekaji wa alama pekee, na akaelekeza ulinzi uendelee kuimarishwa katika eneo la kilomita za mraba 1,500 zilizowekewa alama.