Back to top

WAZIRI MAVUNDE AKUTANA NA WADAU WA KIMATAIFA INDABA KUVUTIA UWEKEZAJI

10 February 2026
Share

Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde anayeongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Kongamano la Mining Indaba akiongozana na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Msafiri Mbibo na Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Mhe. James Bwana wamefanya vikao vya pembeni Februari 9, 2026 na viongozi, wawekezaji na kampuni kutoka nchi mbalimbali kwa lengo la kuboresha mahusiano, kuvutia uwekezaji na kukuza sekta ya madini nchini Tanzania.

Mkutano na Waziri wa Masuala ya Biashara na Uchumi wa Finland Mhe. Sakari Puisto;
Mkutano huu umelenga kuimarisha ushirikiano baina ya Taasisi ya Jiolojia ya Finland (GTK) na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kupitia MoU ili:-
Kuwajengea uwezo watalaamu katika kuchambua, kutafsiri na kuhakiki ubora wa taarifa za Jiosayansi nchini Tanzania.

Kujenga uwezo wa watalaamu wa GST katika kuendesha maabara hususan upimaji wa sampuli kwa viwango vya kimataifa.

Kushirikiana kwenye Utafiti wa jiosayansi hususan High Resolution Geophysical Surveys.

Kikao na taasisi mbalimbali kutoka Serikali ya Marekani;
Ujumbe wa Taasisi kutoka Marekani uliongozwa na Naibu Mkurugenzi na Mkuu wa Shughuli za Uendeshaji za Shirika la Maendeleo ya Biashara la Watu wa Marekani (USTDA), Bw. Thomas Hardy.

Mhe. Waziri ameeleza umuhimu wa kufanya tafiti za kina na kusisitiza kuwa ni vyema Serikali ya Marekani ikaweka mkazo katika eneo hili ili kuwezesha uanzishwaji wa miradi mingi kwenye sekta ya madini nchini.

Mkutano na Taasisi ya Rio Tinto yenye uzoefu wa zaidi ya miaka 150 katika sekta;

Uwepo wa miundombinu ya Reli ya Kisasa (SGR) Shirika la Pamoja la Serikali ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Sera ya Madini, mazingira wezeshi ya kibiashara Sekta ya Madini Tanzania yametajwa kuwa miongoni mwa mambo yaliyoivuta Kampuni ya Kimataifa ya Rio Tinto yenye uzoefu wa miaka 150 kwenye shughuli za madini kuonesha nia ya kuwekeza kwenye Sekta ya Madini nchini.