
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama, amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha kuanzia mwezi Oktoba hadi Disemba mwaka 2023, baada ya Mamlaka ya hali hewa nchini (TMA) kutoa utabiri wa mwelekeo wa mvua za msimu wa Vuli , ambao umeonesha uwepo wa El-Niño.
Waziri Mhagama ameyasema hayo Jijini Dodoma, ambapo ameizielekeza kamati za usimamizi wa maafa na sekta, zisisubiri maafa yatokee, bali waanze kutambua maeneo yote hatarishi na yenye viashiria vya kuathirika na maafa na kuanza kuandaa mipango ya kuzuia madhara yoyote yanayoweza kutoka na utabiri huo.
