Back to top

Waziri Mhagama:Wananchi tambueni thamani ya Mwenge wa Uhuru.

12 October 2021
Share

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewataka wananchi kutambua thamani ya Mwenge wa Uhuru na kushiriki shughuli ambazo umekuwa ukihamasisha.

Waziri Mhagama ameyasema hayo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa, Kilele cha Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2021 na kumbukizi ya miaka 22 ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere katika Viwanja vya Mazaina Wilaya ya Chato mkoani Geita.

Waziri alieleza kuwa, shughuli za Mbio za Mwenge wa Uhuru zinazotarajiwa kufanyika tarehe 14 Oktoba, 2021 katika Uwanja wa Magufuli Wilayani humo huku zikiwa zimebeba kaulimbi isemayo; “TEHAMA ni Msingi wa Taifa Endelevu; Itumie kwa Usahihi na Uwajibikaji”.