Back to top

Waziri Mkuu amsimamisha kazi Mhandisi Ujenzi wa H/Wilayaya Morogoro

18 September 2019
Share

Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa ameagiza kusitishwa upauaji wa majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Morogoro na zitafutwe mbao nyingine zenye ubora.

Waziri Mkuu pia ameagiza kung'olewa milango yote ya Kituo cha Afya cha Mkuyuni kutokana na milango hiyo kuwa mibovu licha ya kuwa majengo hayo hayajaanza kutumika.

Kutokana na kasoro hizo, Waziri Mkuu Majaliwa amemsimamisha kazi Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Wilayaya Morogoro, Bwana Brown Undule.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa maagizo hayo baada ya kukagua miradi hiyo na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi pamoja na utendaji mbovu wa baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo.