Back to top

WAZIRI MKUU ASHIRIKI MKUTANO WA 19 WA NAM

19 January 2024
Share

Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa, ameshiriki ufunguzi wa mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi, na Serikali Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM).
 
Mheshimiwa Majaliwa ameshiriki mkutano huo, uliofunguliwa na Rais wa Uganda Mh. Yoweri Kaguta Museveni, akimwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
 
Mkutano huo wa siku mbili umeanza leo Ijumaa, Januari 19, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Ruwenzori, Kampala nchini Uganda.
 
Katika mkutano huo Rais wa Uganda alikabidhiwa rasmi uenyekiti wa kundi hilo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Cuba Miguel Mario Diaz-Canel Bermudez. 


 
Mkutano wa NAM hufanyika kila baada ya miaka mitatu na Mkutano wa mwisho, wa 18 ulifanyika jijini Baku nchini Azerbaljan mwezi Oktoba, 2019. Mkutano huo haukuweza kufanyika tangu mwaka 2019 kutokana na janga la ugonjwa wa COVID-19 lililoikumba dunia.