Back to top

Waziri Mkuu awataka waislamu kutumia mwezi mtukufu kuiombea Tanzania.

02 May 2021
Share

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasisiza waislam nchini watumie Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuibariki Tainzania, viongozi na wananchi wake wadumishe amani na mshikamano.
.
Ameyasema hayo leo  katika Fainali za Mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Qur’an yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yalihusisha washiriki 15 kutoka nchi 11.
.
Pia, Waziri Mkuu ametoa rai kwa waumini wa dini ya kiislam nchini waendelee kuyaishi mafundisho wanayoyapata katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwenye maisha yao ya kila siku.
.
 “Natambua mchango mkubwa wa waumini katika kuienzi na kuitunza amani kwa kufuata miongozo ya viongozi wetu kupitia mafundisho ya Qur’an ambayo hututaka kuepuka kuivuruga amani.”