Back to top

Waziri mkuu azindua safari za reli ya Tanga –Moshi.

20 July 2019
Share

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea treni ya kwanza ya mizigo kutoka Tanga ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa reli ya kutoka Tanga hadi Moshi.

Waziri Mkuu amepokea treni hiyo leo Julai 20, 2019 ambayo iliwasili saa 4:30 asubuhi kwenye stesheni ya Moshi na kukata utepe wa uzinduzi saa 4:32, kisha akapanda kwenye treni hiyo saa 4:33.

Akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Moshi na wengine kutoka mkoa jirani wa Tanga, Waziri Mkuu amesema amefurahi kupokea treni hiyo yenye mabehewa 20 yaliyokuwa na mzigo wa tani 800 za saruji kutoka kampuni ya Saruji ya Tanga. 

 Amesema kama ilivyo kwa mradi wa SGR, njia ya reli ya Tanga - Moshi yenye urefu wa km. 353, ukarabati wake unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na umetekelezwa na wataalamu wazawa.