
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekemea tabia ya baadhi ya maafisa ununuzi wa umma kukubali zabuni za watoa huduma zenye bei ya juu kuliko bei halisi za soko na kuahidi kuwa ataanza na Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) kulishughulikia suala hilo.
.
Waziri Mkuu amesema hayo wakati akizungumza na wataalamu wa ununuzi na ugavi pamoja na wasimamizi kwenye uzinduzi wa Wiki ya Ununuzi wa Umma iliyoanza leo, Mei 05, 2022, katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, jijini Arusha.
