Back to top

Waziri Mkuu Majaliwa awataka wakulima wa korosho kuwa wavumilivu.

08 November 2018
Share

Waziri Mkuu Mhe.Khasim Majaliwa amewataka wakulima wa korosho nchini kuwa wavumilivu na watulivu wakati huu ambao Serikali inatafuta wanunuzi wa zao hilo.

Waziri mkuu amesema hayo bungeni mkoani Dodoma wakati akijibu maswali yaliyoelekezwa kwake moja kwa moja kama inavyofanyika kila siku ya Alhamisi bungeni hapo.

Waziri mkuu amesema serikali ilifanikiwa kufanya hilo kwa mazao ya kahawa na tumbaku hivyo inatumai pia kuwa itafanikiwa pia kwa zao la korosho.

Kwa sasa kumekuwa na hali tete ikikabili zao la korosho kutokana na wakulima kupata mavuno mengi huku kukikosekana soko la kutosha la zao hilo.