Back to top

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa asema hakuna ugonjwa wa Corona nchini.

31 July 2020
Share

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amewahakikishia Watanzania kuwa nchi ipo salama katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona na hakuna mgonjwa hata mmoja wa ugonjwa huo katika hospitali zote hapa nchini na habari zinazoenezwa juu ya uwepo wa ugonjwa huo ni za kupuuzwa.

Waziri Mkuu amesema hayo katika Baraza la Eid Mnazi Moja jijini Dar es Salaam ambapo Swala la Eid el Adhaa iliswaliwa kitaifa.

Kuhusu matukio ya moto unaozuka na kuteketeza baadhi ya shule za sekondari zinazomilikiwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Waziri Mkuu amesema ameagiza serikali ya mkoa wa Dar es Salaam iunge tume maalum ya kuchunguza matukio hayo na hivi karibuni itatawasilisha taarifa ofisini kwake.