Back to top

Waziri Mkuu Ranil, Rais wa muda wa Sri Lanka

13 July 2022
Share

Spika wa Bunge la Sri Lanka amesema Waziri Mkuu Ranil Wickremesinghe ameteuliwa kuwa Rais wa muda wa nchi hiyo ambapo amebainisha kuwa Rais Gotabaya Rajapaksa alimfahamisha kuhusu uteuzi huo chini ya Kifungu cha 37.1 cha katiba ya Sri Lanka. 
.
Hatahivyo, hakuna neno la moja kwa moja kutoka kwa Rajapaksa mwenyewe ambaye ameikimbia nchi hiyo kwa ndege ya kijeshi, huku kukiwa na maandamano makubwa kuhusu mzozo wa kiuchumi.