Back to top

Waziri Mkuu Sri Lanka aandika barua ya kujiuzulu kwa Mdogo wake.

09 May 2022
Share

Waziri Mkuu wa Sri Lanka Mahinda Rajapaksa ameandika barua ya kujiuzulu kwa Rais wa nchi hiyo Gotabaya Rajapaksa ambaye ni mdogo wa Waziri Mkuu huyo.

Maandamano dhidi ya familia hiyo yenye nguvu ya Rajapaksas yameendelea kwa wiki kadhaa, wakitaka familia hiyo yenye ushawishi ijiuzulu kwa kuhujumu uchumi.

Ombi la Rajapaksa la kujiuzulu lilikuja saa chache baada ya wafuasi wa chama chake kuvamia eneo kubwa la maandamano huko Colombo kuwashambulia waandamanaji wanaoipinga serikali na kupigana na polisi ambao walitumia gesi ya kutoa machozi na maji ya kuwasha kuwarudisha nyuma.