
Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa, amewataka wakulima zao la korosho wafanye kilimo cha kibiashara, kwa kuacha kuuza korosho ghafi na badala yake, wauze zilizobanguliwa ili kujiongeza tija zaidi.
Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akiongea na wananchi wa halmashauri ya Mji wa Newala, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mtwara.
“Wakati wa kubadilika umefika, tutumie fursa hii kujenga viwanda vya kubangulia korosho na kuwawezesha wakulima kubangua na kuuza katika masoko ya nje na ndani".Mh majaliwa.
Amesema bei ya kilo moja ya korosho iliyobanguliwa ni takribani shilingi 13,000 na ghafi ni takribani shilingi 2,000, ukibangua kilo nne za korosho ghafi unapata kilo moja ya ya korosho iliyobanguliwa.
Aidha, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho watoe nafasi kwa wakulima kwenda kubangua korosho zao na kuwatoza gharama za ubanguaji.
