
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa, amewataka wananchi kuacha tabia ya kuvamia maeneo na badala yake wafuate taratibu za kupata ardhi.
Waziri Silaa amesema haiwezekani kutengeneza taifa ambalo wananchi wanajichukulia sheria na katika kipindi anachohudumu wizara ya ardhi atahakikisha anasimamia sheria na kutenda haki katika utendaji kazi wake.
"Tufuate sheria na kuacha kabisa tabia ya kuvamia maeneo ili kuepuka miogoro ya ardhi"Amesema Silaa.
Silaa ametoa kauli hiyo mkoani Morogoro, wakati akizungumza na watumishi wa sekta ya ardhi wakati akifuatilia utekelezaji wa Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975.
