Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. George Boniface Simbachawene ameagiza mamlaka ya bandari kutoa taarifa ya makontena 38 ya chuma chakavu yaliyosafirishwa nje ya nchi licha ya yeye kuzuia.
Akizungumza katika ziara yake bandarini jijini Dar es Salaam kukagua makontena ya chuma chakavu ambapo ameitaka NEMC kusimamia alitoa magizo makotena hayo yasisafirishwe hadi ajiridhishe.